Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewashinda watia nia wenzake 12 wa Ubunge jimbo la Nzega Mjini – CCM kwa kura 367 kati ya kura 376 zilizopigwa, sawa na asilimia 97.

Waziri William Lukuvi ameibuka kidedea katika kura za maoni Jimbo la Isimani, Iringa – CCM baada ya kujizolea kura 453.

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo anayetetea kiti cha ubunge jimbo la Kisarawe ameshinda kwa kura 588 kati ya kura 601 zilizopigwa.

wengine waliokuwa kwenye kinyang’anyiro ni Hassan Bangusilo kura 1, Fransis Gosbert kura 1, Mohamed Masenga kura 1, Ally Goha kura, Zemba Mumbi kura 2, Zainabu Zowange kura 2. na Chaulembo kura 3.

Tulia, Zungu, Hawa Ghasia, Mhagama wapeta kura za maoni
Parimatch kuwapa fursa mpya wateja wake