Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeweka mpango mkakati wa kuandaa vikao vya wadau mbalimbali ya siasa na Jeshi la Polisi ili kutengeneza maelewano kwa lengo la kuondoa changamoto zinazojitokeza baina yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 20, 2021 Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amesema nia ya vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama vya Siasa.

Aidha Jaji Mtungi amesema kikao cha kwanza Cha wadau kitafanyika Septemba 23 mwaka huu ambapo ofisi hiyo itakutana na Jeshi la Polisi nchini kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

Katika hatua nyingine Jaji Mutungi, amesema kuwa Octoba 13 mwaka huu baraza la vyama siasa litafanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar ambapo utashirikisha wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa.

“Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye anamafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano,” Amesema jaji Mutungi.

Aidha Vikao hivyo vimekuja ikiwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia.

Wafugaji kuanza kuvuna mifugo kwa tija
Shahidi kesi ndogo ya mbowe atoa ushahii