Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Klabu ya Young Africans  Jerry Muro amesema kuwa uongozi wa timu hiyo umeshawabaini watu wote wanaotaka kuhujumu uchaguzi.

Muro ameeleza hayo mapema leo na kusisitiza kuwa kuna viongozi wa TFF ambao wanashirikiana na watu wasio wema serikalini wanaotaka kupangua uchaguzi huo.

Amesema kuwa taarifa wanazo na ushahidi wa video na sauti na kama watu hao hawata acha tabia hiyo atawaweka adharani.

“Kama wanabisha wabishe alafu nitaitisha mkutano wa waaandishi wa habari kesho ni waanike mchana kweupe”amesema Muro

TASWA Yatangaza Kamati Ya Tuzo Za Wanamichezo Bora Tanzania 2015-16
Waziri Mkuu: Malikale zitumike kuondoa umasikini