Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio la mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mariam kujeruhiwa kwa risasi, katika eneo la Sinza Lion, ambapo limesema kuwa ilimpata kwa bahati mbaya wakati Askari wakipiga risasi juu kuwatawanya wananchi waliokuwa wanampiga mwizi aliyedaiwa kuiba simu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, leo Mei 20, 2022 wakati akizungumza na East Africa TV ambapo ametolea ufafanuzi wa madai yaliyotolewa na mashuhuda wa tukio hilo kwa kusema kwamba mwanamke huyo aitwaye Mariam amejeruhiwa na polisi.

“Ni kweli tukio hilo limetokea na jeshi linaendelea kulifuatilia, lakini ni kwamba askari walifyatua risasi juu katika juhudi za kumuokoa mtuhumiwa na kwa bahati mbaya kuna mwanamke amejeruhiwa ingawa anaendelea vizuri,” amesema Kamanda Muliro.

“Huyo mtuhumiwa hatujamtambua kwa sababu hajaweza kuongea, alikuwa tayari amepigwa, hawezi kuongea, hivyo tunalichunguza tukio hilo”. amesema Muliro

Barbara Gonzalez, Haji Manara waitwa TFF
Dkt. Maboko: Wanaume wako nyuma kujitokeza kupima VVU