Serikali ya Ubelgiji imerejesha nyumbani sehemu pekee iliyosalia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Congo Patrice Lumumba baada ya miaka 61 tangu kifo chake ambaye aliuawa mnamo mwaka 1961.
Sanduku lililokuwa na jino la dhahabu la shujaa huyo wa uhuru wa Congo lilikabidhiwa kwa familia yake katika hatua ya kutaka kupatanisha mataifa hayo mawili kuondokana na hali ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya mataifa hayo mawili.
Baada ya kuuawa mwaka 1961, mwili wa Lumumba ulizikwa kwenye kaburi lenye kina kirefu kabla ya kufukuliwa na kusambaratishwa kwa tindikali kiasi cha kubakia jino pekee.
Inaelezwa kuwa mmoja wa maafisa aliyehusika na kuagwa kwa mwili wa Lumumba alinyakua jino hilo ili kuhifadhiwa kama kumbukumbu.
Hatua hiyo ya Ubelgiji imekuja wakati nchi hiyo ikijaribu kufidia hukumu ya kikatili iliyowawekea watu wa Congo katika enzi ya ukoloni kufuatia miaka mingi ya kukana ukiukwaji wa haki za binadamu
Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia baada ya uhuru wa nchi hiyo, aidha muda wake wa uongozi ulikuwa mfupi kutokana kwake chini ya miezi mitatu.
Jino la Lumumba litawekwa kwenye sanduku ambalo litahifadhiwa kwenye jeneza, kisha litatembezwa nchi nzima kwa ajili ya kutazamwa kabla ya kuzikwa katika Ikulu ya Kinshasa.
Waziri Mkuu wa sasa wa DRC, Jean-Michel Sama Lukonde, ameeleza kuwa mauaji ya Lumumba kuwa yanaumiza sio tu kwa familia ya Lumumba bali nchi nzima kwa ujumla.