Aliyekuwa naibu spika wa Bunge la 10, Job Ndugai amechaguliwa rasmi na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la 11 kuwa Spika wa Bunge hilo.

Ndugai ameshinda kwa kishindo katika kinyanyang’anyiro hicho kwa kupata asilimia 70 ya kura zote. Ndugai alifuatiwa na Goodluck Ole Mideye wa Chadema, aliyekuwa akiwakilisha vyama vya upinzani vinaunda Ukawa.

Wagombea wa nafasi hiyo walipewa nafasi na Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge na walimpongeza Ndugai kwa kushinda nafasi hiyo.

Mama wa Gaidi aliyejitoa Mhanga Ufaransa Amzungumzia Mwanae
Ali Kiba Aeleza Kwanini Hakupost Kumpongeza Diamond, Vanessa