Mkali wa ‘Mwana’, Ali Kiba amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kutoweka kwenye ukurasa wake post yoyote ya kuwapongeza wasanii wenzake Diamond na Vanessa walioshinda tuzo za AFRIMMA 2015 juzi usiku.

Akiongea katika kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Ali Kiba alieleza kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu hata yeye hufanya mengi na hapongezwi.

Diamond AFRIMMA

Siwezi ku-post kitu kuhusu Kushinda Kwao, unajua hakuna uzalendo. watu wangapi wanafanya Vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo,” alisema.

“Unajua watu mimi hawanijui Wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzuri,” aliongoza.

Hata hivyo, Ali Kiba alitumia muda huo aliokuwa akiongea na Diva The Bawse,  kumpongeza Diamond kwa kushinda tuzo tatu za Afrimma na kueleza kuwa hana tatizo naye.

“Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida tuzo 3, nampongeza Sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa ni Kitu poa Sana… Mimi na Diamond we are good.”

Ali Kiba ambaye alishindwa kupata tuzo ya AFRIMA licha ya kutajwa kuwania vipengele vinne, pia alielezea uamuzi wake wa kufuta post yake ya jana kwenye Instagram aliyoiandika kwa madai kuwa aliona watu wameitafsiri vibaya.

Post yake ilikuwa ikisomeka, “Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #kingkiba.”

Ali aliifuta baada ya kukosolewa vikali na mashabiki wa Muziki.

 

Job Ndugai Achaguliwa Rasmi Kuwa Spika wa Bunge la 11
Wachimbaji Watano Waokolewa Baada Ya Kuishi ‘Kimiujiza’shimoni Siku 41 Wakila Mende