Beki wa pembeni wa FC Barcelona Jordi Alba, yu mashakani kuukosa mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Real Madrid, ambao utaunguruma katika uwanja wa Nou Camp.

Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya FC Barcelona imeeleza kuwa, Alba anakabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu pamoja na goti.

Alba alicheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Real Sociedad ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja, lakini jana alikosa mazoezi ya kikosi cha FC Barcelona, hali ambayo ilimlazimu kufanyiwa vipimo.

Majibu ya vipimo, yalibaini ana tatizo katika kifundo cha mguu pamoja na goti la mguu wake wa kulia, na bado haijaelezwa atajiuguza kwa muda gani.

Alba ataukosa mchezo wa kesho ambapo Barca watakua wanatetea ubingwa wa kombe la Mfalme (King’s Cup) kwa kupambana na klabu ya Alicante inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania.

Chadema waja na oparesheni ‘Kata Funua’
Video: Profesa Ndalichako apingwa kila kona, Chadema sasa ni 'Kata Funua'...