Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anataka kutimiza ndoto yake kwa kumaliza miongoni mwa timu nne bora mwishoni mwa msimu huu.

Mabingwa hao wa ligi ya England, wako katika nafasi ya 14 wakiwa pointi 14 nyuma ya timu inayoshikilia nafasi ya nne.

”Pengine tuna fursa ya kufanikisha ndoto hii kwa kumaliza katika nafasi ya nne,ijapokuwa inawezekana lazima tujaribu”,alisema Mourinho.

Jumatatu Chelsea inaelekea kukabiliana na Leicester katika ligi kuu ya England.

Kufanya vibaya kwa Chelsea msimu huu, kumezua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo, lakini Jose Mourinho amesema ana hakika atasalia kuwa kocha huko Stamford Bridge.

CAF Waitega Dar es salaam Young Africans Ligi Ya Mabingwa
Louis Van Gaal Ajipoza Kwa Kujipa Matarajio