Polisi Tanzania Leo tarehe 26.07.2022 imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Joslin Sharif Bipfubusa toka nchini Burundi mwenye leseni daraja A inayotambulika na CAF na Diploma ya ukufunzi.

Mwalim Joslin anakuwa kocha wa tatu kwa Polisi Tanzania tangu kupanda kushiriki Ligi kuu msimu wa 2010/20 akiwa ametanguliwa na mwalimu Suleyman Matola na Malale Hamsini ambaye mkataba wake ulisitishwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufikiwa hivi karibuni.

Kocha Joslin amesaini mkataba wa kukinoa kikosi cha maafande wa Polisi Tanzania mbele ya Mwenyekiti wa timu Kamishina wa Polisi Charles Mkumbo Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Polisi Tanzania imeingia makubaliano nae baada ya kupitia CV za makocha mbalimbali na kuridhishwa na CV ya mwalimu Joslin ambaye kwa nyakati tofauti amecheza mpira kwenye vilabu vya OC Muungano ya DRC, MP FC, Kibuye FC, KIST FC za Rwanda, Atheletico na Vitalo za Burundi.

Aidha amecheza kwenye timu ya taifa ya Burundi na kufundi timu ya taifa ya nchi hiyo ikiwemo ya U23. Kwa upande wa vilabu amefundisha Bumamuru FC, Messager Ngozi na Aigle Noirc za nchini Burundi.

Kiungo wa Ismailia aishawishi Simba SC Misri
Uzee wa Odinga ni ukomavu wa huduma-Karua