Hatimaye Msemaji wa Klabu ya Young Africans Haji Manara ameweka wazi yaliyotokea kati yake na Rais wa TFF Wallace Karia, wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ uliopigwa Julai 02, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Jumatano (Julai 21) Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ilitangaza kumfungia Haji Manara kwa miaka miwili na kumtoza faini ya Shilingi Milioni 20.

Manara leo Jumatatu (Julai 25) amezungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam na kuanika wazi mazingira ya tukio lililotokea kati yake na Rais Karia, akidai yaliyozungumzwa hayakua sahihi dhidi yake hadi kufungiwa kwa muda wa miaka miwili.

Haji amesema: “Wakati wa half time ya Fainali ya #ASFC nilikuwa nikiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha maana nilikuwa najiandaa kuondoka Pressure ya mpira ilkuwa kubwa, wakati tunaendelea kuongea hatujamaliza hata dakika moja na pale kulikuwa na viongozi wengi, ghafla bila kutarajia wala sikujua imetoka wapi Rais wa TFF kwa ukali na makelele mengi alinifuata akaniambia wewe toka hapo, ondoka hapo.

“Nilikuwa naongea na Mkuu wa mkoa wakati ananinyooshea kidole na kunipgia makelee anawaangalia viongozi wa Coastal Union, nikamwambia nimefanya nini, akaniambia nimekwanbia ondoka ujue hapa kafa mtu, nikamwambia why kila siku unakuwa hivi, kwanini unapenda kufoka, Mkuu wa mkoa na viongozi wakanitoa nikaondoka.

“Baadaye akawa ananifuata nilipo akawa ananiambia nimekwambia hapa ondoka mimi ndiyo rais wa mpira, nikamwambia hiki unachokifanya sicho, imekuwa ni desturi, hunifanyii hivi kwa mara ya kwanza huoni heshima yangu unaishusha?,” Msemaji wa Yanga, Haji Manara.

Geita Gold yapewa mchongo CAF
Simba yaomba radhi makosa ya kiuandishi