Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya wamewapokea madiwani 8 kutoka CUF leo Mei 16.

Madiwani hao 8 wa kata 8 wilayani Tunduru pamoja na kada maarufu KIOSA KIOSA wametangaza kuachana na Chama Cha Wananchi CUF na kujiunga na CCM rasmi.

Wakizungumza mbele ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, wamesema kuwa wamefanya uamuzi huo kwa sababu wanahitaji chama imara kitakachowasaidia kutumikia wananchi kwa utulivu na mienendo inayooeleweka.

Madiwani hao wanatokea kata za Majengo, Nalasi Magharibi, Nandembo, Mlingoti Mashariki, Ligunga, Tinginya na Nakapanya.

Hayo yamejiri ikiwa imesalia miezi kadhaa kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu unaohusisha nafasi ya Rais, Wabunge pamoja na Madiwani.

Dante: Nitapambana na kumshawishi kocha
OSHA watoa msaada vifaa kinga dhidi ya Corona kwa wasioona