Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mbuge anachukua nafasi ya Meja Jenerali Martin Busungu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Akiba.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo  wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam.

Awali Aprili13, Rais Magufuli alimpandisha cheo Brigedia Jenerali Mbuge kutoka kuwa Luteni Kanali na kuwa Brigedia Jenerali.

Dk. Magufuli alimpandisha cheo hicho Brigedia Jenerali Mbuge baada ya kufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwamo ujenzi wa ukuta wa Mirerani.

Video: Mwakyembe aitabilia mema Taifa Stars 'itafuzu kombe la Dunia'
Mtibwa Sugar yaapa kuifunga Simba