Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam utakaogharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019.
Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 20, 2017 wakati akitoa hotuba kabla ya kuweka jiwe la msingi la barabara za juu eneo la Ubungo, ambapo ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo bilioni 1.9 inatoka Serikalini na bilioni 186 inatoka Benki ya Dunia na ivyo ni muhimu kuulinda kwani ni pesa za Watanzania walipa kodi.
 
“Tutasimamia pesa hizi kikamilifu ili tujenge barabara izi za juu vyema,nawataka Watanzania kusimamia mradi huu ili ukamilike haraka na hivyo Wizara,Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ili ulete ukamilike na kuleta tija kwa wananchi hawa”, amesema Rais Magufuli.
 
Rais Magufuli amemuomba Rais wa benki ya Dunia  kuendelea kuikopesha Tanzania katika miradi mingine, kwani Tanzania inapata mkopo huo  kwa sababu inaaminika katika kukopesheka na kurudisha kwa wakati.
 
Amesema kuwa mkopo huu kutoka benki ya Dunia una riba ya asilimia 0.5 na unalipwa ndani ya miaka 40 ivyo ni vyema kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia.
 
Aidha, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kulipa kodi ili Serikali iendelee kutekeleza miradi mingine.
Amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa sura ya pekee ya jiji la Dar es Salaam na kupunguza msogamano wa magari kwa kiasi kikubwa sana.
 
Naye Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim ametoa shukurani kwa Serikali ya Tanzania, amesema kuwa ameshawishika kuja nchini baada ya kusikia vongozi wengi wa Dunia wakisifia jitihada za Rais Magufuli za kuunda upya Serikali yake ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi na kuwekeza katika kujenga miundombinu na elimu.
“Tanzania inaelekea kuwa Taifa la watu wa kipato cha kati miaka nane ijayo na kila mtu kuwa na bima ya afya,elimu bora na muono mzuri wa mbeleni,na njia pekee ya kufika huko ni kujitegemea na kutumia rasilimali za nyumbani katika mkakati bora kabisa na hivyo kupunguza kabisa misaada ya nje ambayo imeshuka hapa nchini kwenu,”Aliongeza Dkt.Jim Yong Kim
 
Ameeleza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kufanya kazi pamoja na Tanzania katika maendeleo.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 21, 2017
Bristol whos who online registry review