Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Uganda ikiwa ni ziara ya pili nchini humo tangu aingie madarakani baada ya kuchaguliwa kuwa Rais.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo Nje imesema kuwa Rais Dkt. Magufuli atawasili nchini Uganda Novemba 9, 2017 na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni kwaajili ya ziara.
Aidha, Rais Magufuli akiwa nchini humo atashuhudia utiaji wa saini mbalimbali huku akitembelea maeneo tofauti tofauti nchini humo kwaajili ya kujione shughuli mbali mbali za maendeleo.
Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli imekuja mara baada ya nchi kuimarisha uhusiano uliokuwepo tangu hapo awali hivyo kuchochea shughuli za maendeleo ikiwemo bomba la mafuta.
-
Majaliwa aitaka Lindi kujipanga kwa ajili ya Baraza la Maulidi kitaifa
-
RC Wangabo “Hakuna Mwandishi wa habari atakayefungwa wala kuzuiwa kufanya kazi yake,”
-
Video: Siri Bombardier nje, JPM hakamatiki
Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli kwa mara ya mwisho kufanya ziara nchini Uganda ilikuwa mwezi Mei 2016 alipokwenda kuhudhuria kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.