Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamad Doha, Qatar akiambatana na mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake.

Rais Dkt. Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu, la Uchumi linalofanyika jijini Doha.

Jukwaa hilo, linatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washiriki ikiwa ni pamoja na viongozi wa kampuni kubwa duniani, viongozi wa juu wa Serikali, na pia mamlaka zinazohusika za Qatar.

Sakata la ubaguzi wa rangi La Liga
10 wafariki kwa Kipindipindu, waliolazwa watajwa