Wakati tume ya uchaguzi ya Taifa (NEC) ikiendelea kutangaza matokeo ya urais, mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji amewasilisha pingamizi rasmi na kuiondoa Chadema katika zoezi la utangazaji wa matokeo ya urais yanayoendelea.

Awali, Duni alifika katika eneo la ukumbi wa Julius Nyerere wakati zoezi likiendelea akidai kuwa amefika kuwasilisha hati ya pingamizi ya matokeo lakini walinzi walimzuia.

Hata hivyo, Duni alifuata maelekezo ya walinzi hao na kuwasilisha pingamizi na kuondoa ushiriki wa Chadema katika matangazo ya matokeo yanayoendelea.

Chadema na vyama vinahyvounda Ukawa walipinga utaratibu wa utangazaji matokeo unaoendelea kwa madai kuwa kura zinazotangazwa haziendani na kura zilipatikana katika baadhi ya vituo hivyo zoezi hilo limelenga katika kumpendelea mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Urais, Kinana Azungumza
Yanaisha Tanzania, Sasa Ni Zamu Ya FIFA