Ni nani ambaye anapambana kutafuta mafanikio bila kufikiri pahala sahihi pakuishi?..yupo kweli?,

Kilicho wazi ni kuwa wengi wetu ni wenye kupambana kuishi maisha ya ndoto zetu ikiwa ni pamoja na kuishi kwenye mijengo ya ndoto zetu na kumiliki vitu mbali mbali vya thamani.

Sasa kutoka New york nchini Marekani mwanamuziki Balcalis Marlenis Almanzar maarufu Cardi B mwenye umri wa miaka 29, amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kumiliki nyumba ya kifahari, aliyokuwa akitamani kuwa nayo kwa miaka mingi hasa katika jiji la New York nchini Marekani.

Nyota huyo amethibitisha hilo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo amebainisha wazi kuwa mpaka sasa anamiliki jumla ya nyumba tatu katika Miji tofauti tofauti nchini huo.

“Mimi na mume wangu wakati wote tumekuwa na ndoto ya kuwa na nyumba katika jiji la New York, na tumeamua kuongeza andiko letu kwa kumiliki nyumba, sasa tuna nyumba Atlanta, Los Angeles pamoja na New York, ninaweza kuwa na kila kitu nikiwa pamoja na familia yangu wakati wote”ameandika Cardi B.

Cardi alidokeza kwenye nukuu yake kwamba sasa ndoto yake imekuwa kweli, kwa kuwa ameweza kumuliki nyumba yake mwenyewe kwenye mji wa nyumbani.

“Siku hizi siishi sehemu moja tu, niko kila mahali kutokana na kazi yangu, Jambo moja nilihitaji ni kuwa na nyumba katika jiji langu la nyumbani la New york”aliongeza.

Caridi B amemshukuru pia mumewe rapa Offset kwa kuziunga mkono jitihada zake mpaka kufikia hatua ya kufanikisha hilo.

Wanandoa hao ambao kwa sasa wana jumla ya watoto wawili Kalture Kiari mwenye umri wa miaka 3 na mwingine mdogo mwenye umri wa miezi mitatu walifunga ndoa mnamo mwaka 2017.

Rais Samia arejea kutoka Glasgow Scotland.
Shahidi wa Jamhuri awekewa pingamizi kesi ya kina Mbowe