Mwawakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake watatu wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na makosa ya ugaidi wamemwekea pingamizi shahidi wa sita wa upande wa mashtaka, huku wakiiomba Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iamuru sehemu ya ushahidi wake ambao ameshaanza kuutoa uondolewe kwenye kumbukumbu za mahakama hiyo.

Pigamizi hilo limewasilishwa kupitia kwa wakili Jeremiah Mtobesya, mara baada ya shahidi huyo wa sita, Sebastian Madembwe, kuanza kutoa ushahidi wake Mahakamani hapo.

Aidha Wakili Mtobesya, amesema kuwa upande wa mashtaka kama wakitaka kumtumia katika mazingira hayo walipaswa wawasilishe maombi rasmi chini ya kifungu cha 289 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), lakini hawajafanya hivyo.

“Pia tutaomba maelekezo kuhusu ushahidi wake ambao umeshaingia iwapo upande wa mashtaka watawasilisha maombi hayo na mahakama ikaridhia.”, amehoji Wakili Mtobesya.

Kiongozi wa Jopo la waendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando akijibu hoja ya pingamizi hilo, ameiomba mahakama hiyo iitupilie mbali pingamizi hilo akidai kuwa halina mashiko ya kisheria.

“Mheshimiwa Jaji pingamizi hilo halina mashiko youote kisheria. Kwanza limeletwa katikati ya ushahidi Ni kinyume cha utaratibu kabisa. Kama wangekuwa na hoja hiyo walitkiwa kuitoa mapema. Pengine ni matokeo ya kutokufuatilia mwenendo kwa umakini.”, amesema wakili Kidando

Wakili Kidando amesema kuwa kiini cha ushahidi huo kilisomwa katika mwenendo wa shauri hilo katika mwenendo wa Agosti 23, 2020.

“Lakini pia katika ile orodha ya vielelezo nyaraka anayokuja kuizungumza (maelezo yake ya maandishi) imeorodheshwa namba 18 na imesainiwa naye shahidi, Sebastian Madembwe SSP.”, ameongeza wakili Kidando

Naye, Wakili Mtobesya amedai kuwa upande wa mashtaka wamemshambulia kuwa hakuwepo tangu mwanzo, lakini akasema kuwa wanachokifanya ni kusaidia mahakama, hivyo kutokuwepo kwake tangu mwanzo hakuondoi uhalali wa hoja yake.

“Kwenye commital proceedings hakuna substance ya ushahidi wake. Substance Kuna vitu vitatu. Kwanza jina lake, hatukatai lipo lakini statement yake haipo, kuwa anakuja kusema nini. Statement hiyo ni ya muhimu sana.”, amesisitiza Wakili Mtobesya na akaomba mahakama itoe mwongozo kuhusu hilo.

Hata hivyo, Jaji Joachim Tiganga baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo kwa muda kwa ajili ya kuandika uamuzi.

Jumba la Kifahari la Cardi B Marekani.
Khaligraph Jones amtupia Ali Kiba kwenye hii.