Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amemwambia mshambuliaji wa Klabu hiyo Super Mario Barwuah Balotelli afanye kila linalowezekana ili afanikishe mpango wa kusaka mahala pa kucheza kuanzia msimu wa 2016-17.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Italia, alipelekwa kwa mkopo AC Milan msimu uliopita na sasa amerejea mjini Liverpool kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25,  amefanikiwa kupachika mabao manne tangu alipojiunga na Liverpool mwaka 2014 akitokea AC Milan.

“Hayupo kwenye kiwango bora kwa sasa kuweza kugombania namba na watu wawili au watatu tunahitaji mtu aliye tayari, lakini kuna vilabu vinamuhitaji sana Mario nadhani anaweza kwenda huko” alisema Klopp.

Video: Waziri Nape Ayafutia Usajili Magazeti 473
Mwingine Wa Ivory Coast Kufanyiwa Majaribio Azam FC