Meneja wa klabu bingwa England, Liverpool FC, Jurgen Klopp amesema wachezaji wake wanatakiwa kujifunza kwa kilichotokea katika mchezo dhidi ya Arsenal ambapo wamepoteza nafasi ya kuvunja rekodi ya Manchester City.

Kikosi cha Klopp ambacho kinatarajiwa kukabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya mchezo dhidi ya  Chelsea juma lijalo,  kilikua na nafasi ya kuvunja rekodi ya misimu miwili iliyopita iliyowekwa na  Manchester City  kwa kumaliza msimu huo wakiwa na alama 100 kibindoni.

“Tunatakiwa kujifunza tena kwa asilimia 100. Tumekuwa na mteremko kabla na ndio maana walituadhibu, hii safi sana kwa sababu tunapaswa kujifunza. Nawapongeza Arsenal walikuwa pale na walitumia nafasi,” alisema Klopp.

Aliendelea, “Siwezi kusema vibaya kwenye jambo chanya, tumepata pointi ambazo tumestahili na tutaona hadi mwisho wa msimu tutakuwa na ngapi. Kuna mambo ambayo sikuvutiwa nayo wakati wa mchezo lakini kiujumla mchezo ulikuwa mzuri.”

“Tulikuwa na mapumziko pengine yamechangia kupoteza kwetu. Huu ndio mpira kuna muda hushangaza, wachezaji nao ni binadamu sio wakamilifu kuna muda hukosea,” alisema.

Licha ya kwamba walikuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa jana  kupitia kwa  Sadio Mane, washika mitutu wa London, Arsenal walitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao yao yalifungwa na  Alexandre Lacazette na Reiss Nelson.

Baada ya kuifunga Liverpool katika mchezo wao uliopita Arsenal watakuwa na kibarua kingine kigumu Jumamosi cha kucheza dhidi ya Manchester City katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.

Upande wao majogoo wa jiji Liverpool  watakuwa na juma moja la kupumzika kabla ya  kuikaribisha Chelsea kwenye Uwanja wao wa Anfield, Jumatano ikiwa ni muendelezo wa michezo ya EPL.

Jose Mourinho awatosa Man Utd, ataja 11 bora
Waziri Junior awatahadharisha Mbao FC