Meneja wa majogoo wa jiji “Liverpool” Jurgen Klopp anatarajiwa kumrejesha kundini mlinda mlango kutoka nchini Hispania Pepe Reina.

Klopp anafanya mipango ya kumrejesha mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 33, kutokana na mapungufu anayoyaona katika safu ya ulinzi ambayo aliikuta ikishikiliwa na kipa kutoka nchini Ubelgiji Simon Mignolet.

Klopp anaamini mlinda mlango huyo, bado ana uwezo wa kukaa langoni mwa Liverpool kutokana na uzofu mkubwa alionao, tofauti na ilivyo sasa ambapo anahisi huenda akaingia majaribuni endapo ataendelea kufanya kazi na Mignolet.

Kwa sasa, Reina ni mchezaji wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich lakini amekua chaguo la pili kutokana na changamoto alizokutana nazo klabuni hapo za kuaminiliwa kwa Manuel Peter Neuer.

Alipokua Anfield kuanzia mwaka 2005 hadi 2014, Reina alikua chaguo la kwanza na aloifanikiwa kucheza michezo 285, kabla ya kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya SSC Napoli ya nchini Italia na kicha kuuzwa FC Bayern Munich mwaka 2015.

Roberto Di Matteo Kukabidhiwa Zigo La The Lions
Martin Skrtel Kuihama Liverpool