Mwanasiasa machachali aliyetambulika zaidi kwa kuibua bungeni sakata la Tegeta Escrow, David Kafulila amefungua rasmi kesi katika mahakama Kuu kanda ya Tabora akipinga ushindi wa Hasna Mwilima (CCM) kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kafulila ambaye aligombea nafasi hiyo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi alifungua kesi hiyo kupitia wakili wake Daniel Lumenyela.

Katika malalamiko yake, Kafulila anadai kuwa msimamizi wa uchaguzi huo alimpora ushindi wake na kumtangaza kwa nguvu mgombea ambaye alikuwa ameshindwa kwa hesabu za kura zote halali zilizojumlishwa kutoka vituoni.

Kafulila anadai kuwa yeye alipata jumla ya kura 34,000 dhidi ya Hasna Mwilima aliyepata kura 32,000 lakini msimamizi wa uchaguzi aliamua kumtangaza Hasna kuwa mshindi.

“Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alichokifanya ni kuchukua matokeo ya kura ya mteja wangu na kumpa Hasna Mwilima wa CCM. Ndio maana walilazimisha kuwepo kwa ulinzi mkali ili watangaze matokeo batili,” alisema wakili Lumenyela.

 

Yaliyomsibu Lowassa Yamchanganya Aliyeokolewa Mgodini Baada Ya Kunasa Siku 41
Urusi, Ufaransa Waivuruga ISIS, Washusha Mabomu Ya Kihistoria