Joseph Bulule, mmoja kati ya wachimbaji wachimbaji watano wa madini waliookolewa baada ya kunasa ndani ya shimo la mgodi kwa siku 41 amezinduka hospitali na kumuulizia Edward Lowassa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Kwa kuwa wachimbaji hao walinasa mgodini tangu oktoba 5 kabla hawajaokolewa mwanzoni mwa wiki hii walikuwa hawafahamu kabisa kinachoendelea nje ya shimo walilokuwa wanaishi kwa miujiza kwa kula mende na magome ya miti, hivyo hafahamu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Nani alishinda katika uchaguzi mkuu, Lowassa alishinda? Maana sisi tangu Oktoba 5 tuliuwa hatujui kilichokuwa kinaendelea,” aliwauliza waandishi wa habari waliofika kumuona katika hospitali ya Wilaya ya Kahama walipolazwa wahanga hao.

Majibu ya waandishi wa habari kuwa Lowassa alishindwa yalionekana kumnyima raha na kumshangaza Bulule, hali iliyoonesha kuwa imani yake kubwa ilikuwa kwa Lowassa kuibuka mshindi lakini hakupata nafasi ya kushuhudia kilichoendelea kwenye kampeni hadi mwisho wa kinyang’anyiro hicho.

Dkt. Magufuli aliibuka na ushindi mnono wa asilimia 59 na kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo. Aliapishwa rasmi na kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivi sasa anatarajia kumteua Waziri Mkuu na baraza la mawaziri.

Taarifa hii ni mpya kabisa kwa wahanga watano wa tukio la kufunikwa katika mgodi tangu Oktoba 5 wasijue kinachoendelea huku wakiishi kwa kula magome ya miti na wadudu aina ya mende.

Mrembo Akutwa Na Majanga Haya Alipoenda Kukutana Na Mwaume Aliyemfahamu Facebook
Kafulila Atinga Rasmi Mahakama Kuu