Msichana mwenye umri wa maika 15 ameiweka familia yake katika hali ya majonzi baada kupotea alipoenda kukutana kwa mara ya kwanza na rafiki yake wa kiume aliyemfahamu kupitia Facebook.

Msichana huyo raia wa Uingereza aliyetajwa kwa jina la Kayleigh Haywood mwenye umri wa miaka 15 alimuomba rafiki yake wa kike amsindikize kukutana na rafiki huyo wa Facebook waliyekuwa wana-chart kwa muda mrefu, lakini baadae alitangaza kuwa ameghairi lakini kumbe alikwenda peke yake kwa siri.

“Walikuwa wamepanga kwenda kukutana na huyo mwanaume Ijumaa jioni, lakini ghafla mapema alieleza kuwa hataenda tena kukutana na kijana huyo,” chanzo kiliiambia Daily Mirror.

Kwa mujibu wa Daily Mirror, baada ya kupotea kwa muda, Jumamosi iliyopita simu ya mkononi ya msichana huyo ilikutwa ikiwa imetelekezwa kwenye eneo la hifadhi ya msitu wa Ibstock hali iliyowafanya wazazi wake kuongeza hofu zaidi.

Katika hali ya majonzi, wazazi wa Kayleigh waliwaeleza Polisi kuwa binti yao alikuwa mtu mwema sana na aliyekuwa anawajali sana rafiki zake.

 

 

 

Licha Ya Vitisho Vya Ugaidi, Ligi Za Ufaransa, Hispania Kuendelea
Yaliyomsibu Lowassa Yamchanganya Aliyeokolewa Mgodini Baada Ya Kunasa Siku 41