Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga zinasema kwamba, mshambuliaji wake, Raia wa Liberia, Kpah Sherman anakaribia kutua katika klabu mojawapo inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Winga aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha  Yanga, Mbrazil,  Andrey Coutinho anatafutiwa timu itakayomnunua baada ya BDF XI ya Botswana kutaja dau dogo la shilingi milioni 10 za Kitanzania. Hata hivyo, St.George ya Ethiopia wameonesha kuvutiwa na Coutinho.

Yanga imepanga kumalizana na kiungo mkabaji wa Gor Mahia , Khalid Auch pamoja na mshambuliaji Michael Olunga ambaye Azam FC na Simba SC wanawania saini yake pia.

Beki kiraka, Mbuyu Twite yupo mashakani kuendelea kukipiga Jangwani huku tatizo haswa imekuwa usumbufu kutoka klabu yake ya zamani ya FC LUPOPO.

Urusi Yatahadharishwa Kombe La Dunia 2018
Wema Sepetu Azua Mtafaruku Viti Maalum, Mwenyekiti UWT Atishia Kuhama CCM