Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Ramadhani Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi alichukua nafasi ya Dkt. Wilson Mahera Charles ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kupitia taarifa ya iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka iliyotolewa hii leo Februari 26, 2023 pia imeeleza kuwa Rais Samia amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, akichukua nafasi ya Omary Tebweta Mgumba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Ramadhani Kailima, Mkurugenzi mpywa wa Uchaguzi.

Aidha, Dkt. Francis Kasabubu Michael ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ambapo kabla ya uteuzi huo, Dkt. Michael alikuwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia pia amemteua Christina Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – Itikadi
na Uenezi.

Ulega Waziri mpya Mifugo na Uvuvi
Panga pangua ya Rais Samia