Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa mitatu ya Shinyanga, Tanga na Songwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Februari 26, 2023 na Kurugenzi ya mawasiliano Rais Ikulu imeeleza kuwa Rais amemteua Christina Mndeme, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ambaye alichaguliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amehamishiwa Mkoa wa Tanga na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Omary Mgumba uteuzi wake ukitenguliwa.

Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael nae ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Kailima ateuliwa Mkurugenzi wa Uchaguzi
'Mwana FA' Naibu Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo