Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Katika mabadiliko hayo, David Silinde sasa anakuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na akimpisha Deogratias Ndejembi kuwa Naibu Waziri nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mashimba Ndaki, uteuzi wake umetenguliwa.

Kupitia mabadiliko ya Manaibu Waziri, Rais Samia pia amemhamisha Paline Gekul toka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba kuchukua nafasi ya Geofrey Pinda aliyehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha katika mabadiliko hayo, pia Rais Samia amehamishia majukumu ya Uwekezaji katika Ofisi ya Rais na kufuta nafasi ya Katibu Mkuu (Uvuvi), ambapo sasa Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakuwa na Katibu Mkuu mmoja na Naibu makatibu wawili.

Uchaguzi Nigeria: Kura zahesabiwa, mchuano mkali
Kailima ateuliwa Mkurugenzi wa Uchaguzi