Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele, Parokia ya Kimiza, Jimbo la Kayanga wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera jana usiku liliteketezwa kwa moto na watu ambao bado hawajafahamika.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kanisa hilo lilichomwa moto jana usiku lakini ilibainika mapema asubuhi huku mali zote zilizokuwa ndani zikiteketea.

Askofu wa Jimbo la Kayanga, Almachius Vicent Rweyongeza alilaani tuko hilo na kuwataka waumini wa Kanisa Katoliki kuwa watulivu na kutopanga kulipa kisasi hata kama watawabaini waliotekeleza tukio hilo baya.

Naye Paroko wa Kigango hicho, Padri Fortunatus Bijura amewataka waumini kutokata tamaa na kwamba waendelee kusali kwani hata chini ya miti watafanya ibada.

Ofisa Upelelelezi wa Wilaya hiyo, Masoud alitoa wito kwa wananchi kudumisha ulinzi shirikishi kwa kuunda vikundi vya ulinzi pamoja na kutoa taarifa haraka Polisi ili kupambana na uhalifu.

Young Africans Hatarini Kupoteza Huduma Ya Kocha
Familia Ya Haji Mwinyi Ngwali Kulishtaki Gazeti Mahakamani