Kanisa la International Pentecost Holiness limebariki ndoa za wanaume wenye wake wengi zaidi ya 800, ambazo ni za kawaida katika baadhi ya jamii za Kiafrika, ambapo Kiongozi wa Dhehebu hilo anadai zimeidhinishwa na Biblia.

Wanandoa hao walibarikiwa Jumapili ya Pasaka (Aprili 9, 2023), katika moja ya sherehe kubwa za harusi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo Misa ya wanandoa wengi hufanyika mara tatu kwa mwaka, siku ya Pasaka, mwezi Desemba na wakati wa maadhimisho ya mwezi Septemba ya kuanzishwa kwa kanisa hilo mwaka 1962.

Lebogile Mamatela, mwenye umri wa miaka 38, ambaye ni mfanyakazi wa serikali ambaye amekuwa mke wa pili kwa baba wa binti yake baada ya hafla hiyo amesema, “ni siku isiyo ya kawaida, nina furaha sana. Ninathamini sana wakati huu kwa kuwa miongoni mwa familia ya Mahluku. Ni hisia nzuri.”

Naye Mume wake, Roto Mahluku mwenye umri wa miaka 40, aliyejiunga na kanisa hilo mwaka 1993 na alimuoa mke wake wa kwanza, Ditopa Mahluku miaka 16 iliyopita alisema ni “ni furaha kubwa maana leo hii nina watoto watatu na ni fahari sasa kuona muunganiko wa kiimani.

Papa Francis aombea amani, ataka watu kuaminiana
Watu 30 wauawa katika shambulio kambi ya wakimbizi