Chama cha soka nchini England (FA), kimethibitisha kuanza kufanya uchunguzi wa kauli iliyotolewa na meneja wa Man Utd Jose Mourinho, mara baada ya kikosi chake kupata bao la ushindi, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Newcastle United uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mourinho anadaiwa kutoa maneno machafu mbele ya kamera iliyokua imemuelekea na ushahidi wa awali umebainisha kuwa, alitamka kauli ya “sons of b*****s” (Watoto Wa Makahaba).

Uongozi wa FA umesema utaomba msaada kwa watu maalum wanaojua kusoma midomo, ili kufahamu kwa undani kauli iliyotolewa na meneja huyo kutoka nchini Ureno.

Mshambuliaji kutoka nchini Chile, Alexis Sanchez aliifungia Man Utd bao la tatu na la ushindi dakika za lala salama katika mchezo huo, ulioshuhudia Man Utd wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao mawili kwa sifuri.

Mabao mengine ya Man utd katika mchezo huo yalifungwa na Juan Mata pamoja na Anton Matial.

Kwa upande wa Newcastle United, mabao yao yalifungwa na Kenedy na Yoshinori Muto.

Sumaye: Dkt Bashiru ajiandae kuchukiwa CCM
Video: Chukua tahadhari katika bichi hizi, ni hatari kwa maisha yako