Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umempendekeza kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kuwania wadhifa wa spika wa Bunge la Kitaifa.

Muungano huo ambao umepoteza urais kwa Muungano wa Kenya Kwanza, unamtaka Kalonzo kurithi nafasi ya Justin Muturi kama spika baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Mgombea mwenza wa Raila, Martha Karua alisema kuwa wana wabunge wengi waliochaguliwa katika Bunge la Kitaifa kuliko Muungano wa Kenya Kwanza hivyo wana nafasi Kuba ya kupata nafasi ya Spika kwa kura za upande wake.

Azimio Wampendekeza Kalonzo Musyoka Kuwania Nafasi ya Spika wa Bunge la Taifa.

Duru za kisiasa nchini Kenya zinadokeza kuwa Kalonzo ana nafasi nzuri zaidi ya kuchaguliwa kuwa spika kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika sheria na siasa.

Wakili huyo alihudumu kama naibu spika wa Bunge la Kitaifa kati ya mwaka wa 1988 na 1992 wakati wa utawala wa KANU.

Hata hivyo, Raila alikuwa ameahidi kumteua Kalonzo kuwa waziri mkuu katika serikali yake iwapo angeshinda uchaguzi wa urais wa 2022.

Agosti 17, 2022 Rais Mteule William Ruto alifichua kuwa wabunge 10 waliochaguliwa kwa tiketi ya kujitegemea walijiunga na Muungano wa Kenya Kwanza huku vita vya kulidhibiti bunge vikizidi kupamba moto.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza na viongozi waliochaguliwa kupitia vyama tanzu vya Kenya Kwanza katika makazi yake ya Karen, Ruto alisema wabunge hao wataunga mkono ajenda ya serikali yake.

Muungano wa Kenya Kwanza Alliance ulifanikiwa kupata viti 159 katika Bunge la Kitaifa, huku Azimio la Umoja ukiwa na wingi wa viti 162.

DRC yairithi Malawi kuiongoza SADC
Twaha Kiduku: Nitapambana kwa ajili ya watanzania