Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), FĂ©lix Tshisekedi ameshika usukani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wakati wa Mkutano wa 42 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaofanyika Kinshasa kuanzia Agosti 17 na 18, 2022.

Tshisekedi, anachukua nafasi hiyo kumrithi Rais wa Jamhuri ya Malawi, Lazarus McCarthy Chakwera ambaye ametoa wito kwa nchi wanachama kuwa huru kutokana na ushawishi wa nje hasa Jamhuri ya Kenya.

Amesema, “Utekaji nyara ambao tumeruhusu nchi za Magharibi kufanya nchini DRC ni dhambi ambayo lazima tutubu, kusuluhisha na kukataa kuona inarudiwa mahali popote katika eneo letu kwani inaleta athari miongoni mwetu.”

Mkutano huo, umewakutanisha Wakuu wa Nchi 12 wanachama wa SADC na utapitia ajenda za maendeleo katika ushirikiano wa kikanda kulingana na matarajio ya SADC , ambayo yanatazamia kuwa na ukanda wa viwanda, amani, umoja, ushindani, kati hadi wenye kipato cha juu, ambapo wananchi watafurahia ustawi endelevu wa kiuchumi.

Akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Tshisekedi amesema, “Nitakuwa makini katika kutekeleza mipango ya kuendeleza miundombinu na huduma katika kanda ambayo inahusishwa moja kwa moja na mikakati yetu kuu ya kuchochea ushirikiano wa kiuchumi na kuondoa umaskini katika kanda ya SADC.”

Mkuu huyo wa Nchi ya DRC, pia ndiye Rais wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS), na anatajwa kuhusika na makabiliano ya kumaliza mgogoro uliopo baina yake na Paul Kagame juu ya mapigano yanayotokea katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Makalla awakabidhi NSSF eneo lililovamiwa
Kenya: Kalonzo Musyoka kuutwaa Uspika wa Bunge?