Klabu ya Kerala Blasters FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini India (Indian Super League) imetangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspur na Manchester United Dimitar Berbatov.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Bulgaria, mwenye umri wa miaka 36, amesaini mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuwa huru tangu alipoachana na klabu ya PAOK ya nchini Uguriki mwaka 2016.

Kerala Blasters, ambayo inamilikiwa na mchezaji wa zamani wa Cricket Sachin Tendulkar, ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini India msimu uliopita, ikitanguliwa na Atletico de Kolkata ambayo kwa sasa inanolewa na gwiji wa soka kutoka nchini England Teddy Sheringham ambaye mwezi uliopita alimsajili Robbie Keane.

Kerala inanolewa na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Man Utd Rene Meulensteen.

Korea Kaskazini yazidi kuivuruga Marekani.
Ronald Koeman Afurahia Rooney Kustaafu Timu Ya Taifa