Khloe Kardashian ameshindwa kukaa na siri ya muda mrefu inayohusu maisha yake na rapa The Game, wakati mrembo huyo alipokuwa na umri wa miaka 17 tu (mtoto).

Mrembo huyo amefunguka kupitia tovuti yake kuwa aliwahi kuishi na mwanaume mwenye umri mkubwa katika nyumba moja alipokuwa na umri wa miaka 16 na baadae akiwa na miaka 17 aliishi pia nyumba moja na rapa The Game.

Kwa mujibu wake hakukuwa na uhusiano wowote zaidi ya kuwa chini ya paa moja wakishea vyote kasoro chumba cha kulala.

“Nilipokuwa na miaka 16, nilihama nyumbani nikapanga chumba kwenye nyumba ya mwanaume mmoja mkubwa. Lakini msiitafsiri tofauti, hakukuwa na uhusiano ule. Alikuwa ana familia na mimi nilikuwa naishi katika moja ya chumba cha kulala cha nyumba yake,” aliandika Khloe Kardashian.

Aliongeza kuwa alipofikisha umri wa miaka 17, alihamia katika nyumba nyingine ambapo alikuwa anaishi na wanaume wanne ndani ya nyumba hiyo ambapo mmoja kati yao alikuwa rapa The Game.

“Moja kati ya roommates wangu alikuwa rapa The Game. Nilimfahamu tangu nilipokuwa na umri wa miaka 14 na tulikuwa marafiki,” alisema mrembo huyo ambaye ni mdogo wake mke wa Kanye West, Kim Kardashian.

Alisema kuwa wazazi wake hawakutaka aondoke nyumbani akiwa na umri ule lakini kwakuwa alikuwa mkaidi aliamua kujitafutia maisha mapema.

Kiongozi mpya wa Taliban atoa sharti la kwanza kwa Marekani
Makonda atangaza vita iliyomshinda Makamba, Ni muda wa kuishinda