Tajiri wa Klabu ya Chelsea, Todd Boehly ameshindwa kuwahakikishia mashabiki hatma ya timu yao baada ya kuzungumza kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano na Waandishi wa Habari.

Bosi huyo alisisitiza anaamini ufumbuzi utapatikana kufuatia mwenendo mbovu tangu alipomtimua Thomas Tuchel na Graham Potter akafuata.

Hata hivyo licha ya kuwatimua makocha hao The Blues haijaimarika chini ya kocha wa mpito, Frank Lampard ambapo imeporomoka hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa na pointi 39.

Haya yote yametokea licha ya uwekezaji mkubwa kwenye kikosi ambacho kimeshuhudia ada kubwa za uhamisho na mikataba mirefu wakipewa.

Pia kumekuwa na mtafaruku nje ya uwanja huku wachezaji wakidaiwa kugombana wao kwa wao kwenye benchi baada ya kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Arsenal. Lakini bosi huyo wa

The Blues amedai wanachotaka timu ipate matokeo mazuri lakini utakuwa ni mchakato wa muda mrefu mpaka kocha apatikane.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Sky Sports bosi wa The Blues, Todd alisema: “Unajua mashabiki wanataka ushindi. Bado tuna safari ndefu kuelekea katika mchakato huo, lakini kama uongozi tunaamini ufumbuzi utapatikana haraka.”

Kauli hiyo haikuwashawishi mashabiki wa Chelsea waliomjia juu bosi huyo raia wa Marekani aliyetumia fedha nyingi kwenye usajili wa wachezaji.

Shabiki mmoja wa Chelsea aliijibu kauli ya Todd akidai: “Hajui chochote kuhusu soka. Ni mfanyabiashara ambaye anasubiri aingize mkwanja akafurahie, hii ni timu sio mdoli wa kuchezea.”

Mapigano Sudan: Watoto saba hufa kila saa, UN yaonya
Viongozi watakiwa kukagua miradi ya maendeleo