Klabu ya Malaga CF imeonyesha nia ya kutaka kumrejeasha nchini Hispania mlinda mlango Iker Casillas Fernández ambaye aliwahi kutamba akiwa na Real Madrid kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Casillas kwa sasa ni mlinda mlango wa FC Porto ya nchini Ureno, na taarifa zinaeleza kuwa tayari ameshaanza kufanya mazungumzo na uongozi wa Malaga CF kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kurudi nyumbani wakati wa majira ya baridi (Januari Mwaka 2017).

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamepewa baraka na uongozi wa FC Porto ambao umeonyesha kuwa tayari kumuachia Casillas ambaye walimsajili mwaka mmoja uliopita akitokea Real Madrid.

Harakati za kusajiliwa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 35, zinapewa msukumo na mmiliki wa klabu ya Malaga CF Sheikh Al Thani, ambaye anadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Casillas.

Endapo usajili wa mlinda mlango huyo ambaye alikiongoza kikosi cha Hispania kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010 na kisha ubingwa wa Ulaya mwaka 2012, huenda ikawa mtihani mkubwa kwa Idriss Carlos Kameni ambaye ndiye chaguo la kwanza la meneja Juande Ramos.

Kameni amekua mlinda malngo chaguo la kwanza klabuni hapo tangu mwaka 2012 aliposajiliwa akitokea Espanyol.

Algeria Wavunja Mkataba Wa Milovan Rajevac
Baraka The Prince ang'aka tena, Stan Bakora ajibu