Mchekeshaji, Stani Bakora ameibuka na kujibu mashambulizi aliyoendelea kutupiwa na Msanii wa Bongo Fleva, Baraka The Prince kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kufanya cover ya video ya wimbo wake unaotambulika kwa jina la ‘Nisamehe’

Mchekeshaji huyo amemshangaa The Prince kuendelea kumchokonoa kwani ameshatoa kauli kuwa hataki utani naye, pia meneja wake na wa Baraka wamesha ongea hayo, amesema kama hawakulizika na maongezi hayo wangesema na si kuendelea kumsakama.

Kauli hiyo ya Stan Bakora ni kufuatia ujumbe mwingine alioandika Baraka The Prince katika ukurasa wake wa Instgram akimsema mchekeshaji huyo kuwa anajichubua.  

Kibopa Wa Malaga CF Apania Kurudisha Iker Casillas
Obama amvaa Trump, amchongea kwa chama chake