Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imesema ipo katika matayarisho ya kuanza kufundisha lugha ya kichina katika ngazi ya elimu ya sekondari kutokana na umuhimu wa lugha hiyo katika mawasiliano.
Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali, Simai Mohamed amebainisha hayo jana wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la paje, Jaku Hashim aliyetaka kujua lini lugha ya kichina itafundishwa katika ngazi ya sekondari Unguja na Pemba.
Simai amesema wizara ipo katika maamdalizi kwani lugha ya kichina ni muhimu hata pale wanafunzi wanapoenda kupata elimu ya vyuo vikuu nchini China.
“Napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la wawakilishi, tunakusudia kufundisha lugha ya kichina kwa ngazi ya sekondari ili kuweka vizuri wanafunzi wetu watakao bahatika kwenda kusoma china kufahamu vizuri masomo yao” Amesema naibu waziri Simai.
Zanzibar, lugha ya kichina hadi sasa inafundishwa vizuri katika chuo kikuu cha Taifa (SUZA) katika ngazi ya stashahada.