Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amelaani vitendo vya baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kumlisha maneno kwa malengo ya kujiimarisha kisiasa dhidi ya Serikali iliyoko madarakani.

Kupitia mtandao wa Twitter, Dkt. Kikwete amewataka watu wanaotumia picha zake vibaya mitandaoni kwa malengo yao binafsi ya kisiasa kuacha mara moja.

“Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa,” ameandika.

Rais huyo mstaafu amesisitiza kuwa anamuunga mkono Rais John Magufuli na Serikali yake.

Hivi karibuni, baadhi ya watu wamekuwa wakitumia picha fupi za video zinazomuonesha Dk. Kikwete akieleza kuwa uongozi mpya unapaswa kuyaendeleza mazuri yaliyoachwa na Serikali iliyopita na sio kuyabomoa.

kikwete

 

Benki Kuu yachukua usimamizi wa Benki ya Twiga kuinusuru
Video Mpya: Dee Pesa Feat. Jack Chant & Ebe Nation – Kanjubahi