Polisi aliyeonekana katika kipande cha video iliyosambaa hivi karibuni kwenye mitandao ikimuonesha akishawishi na kupokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari moja binafsi katika kijiji cha Kilumbo wilayanai Handeni mkoani Tanga amefukuzwa kazi na anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwambeji, askari huyo anayefahamika kwa jina la Anthony Temu mwenye umri wa miaka 46 ambaye tayari ameshafukuzwa kazi anaendelea kuchukuliwa hatua za kisheria na kwamba atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka wakati wowote.

Kamanda huyo wa polisi ameeleza kuwa Anthony Temu anakabiliwa na kesi  kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa kinyume cha sheria ya Utumishi wa Umma namba 11 ya mwaka 2007, kifungu cha 15. Bw. Temu anadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 9 majira ya saa saba mchana.

 

Mbweha Wa Jangwani Kuwasili Alkhamis
King Kibadeni Akabidhiwa Mikoba Kilimanjaro Stars