Sauti ya wananchi kwenye sanduku la Kura yameongea jijini Dar es Salaam na kuwaacha watu baadhi ya watu midomo wazi husan katika majimbo ya Temeke na Kinondoni yaliyokuwa yanaaminika kuwa ngome za CCM.

Jana, sauti ya msimamizi wa uchaguzi ilirasimisha kung’olewa kwa aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan kwa tiketi ya CCM baada ya kumtangaza Maulid Mtulia wa CUF kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.

mTULIA

Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa na msimamizi huyo, Maulid Mtulia alishinda baada ya kupata kura 70,337 huku Iddi Azzan akipata kura 65,964.

Mtemvu

Katika jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu ameshindwa kutetea kiti chake baada ya msimamizi wa uchaguzi kumtangaza rasmi Abdalla Mtolea wa CUF kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.

NEC Yajibu Malalamiko Ya Ukawa
Matokeo Urais Zanzibar ‘Vutankuvute’, Maalim Seif Anyemelewa