Wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ikisubiriwa kutangaza matokeo ya urais mapema asubuhi hii, sintofahamu imewagubika wananchi visiwani humo hasa baada ya mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif kujitangazia ushindi.

Kuchelewa kutolewa kwa matokeo hayo kumezua hali ya wasiwasi visiwani humo iliyopelekea kuimarishwa kwa ulinzi mkali kupitia jeshi la wananchi.

Wakati Maalim Seif akijihakikishia ushindi na kumtaka mshindani wake Dkt. Ali Shein kukubali matokeo, ZEC kutangaza matokeo mapema pamoja na Rais Jakaya Kikwete kusaidia katika hatua za kukabidhiana madaraka, imeripotiwa kuwa ZEC imelitaka jeshi la polisi kumkamata mgombea huyo kwa kile kilichodaiwa kuwa amekiuka sheria ya uchaguzi kwa kujitangaza mshindi.

Sheria ya Uchaguzi inaipa Tume ya Uchaguzi pekee mamlaka ya kumtangaza mshindi wa nafasi ya urais na mtu anayekiuka sheria hiyo anatenda kosa la jinai.

Ripoti zinaeleza kuwa umeme umekatika katika eneo kubwa la Zanzibar hali inayoongeza wasiwasi zaidi.

Kilichowakuta Abbas Mtemvu, Idd Azzan
Ukawa Wapinga Mwendendo wa Matokeo ya Urais, wataka vijana wao Waachiwe