Kocha Mkuu wa Taifa stars, Kim Poulsen ameridhishwa na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar katika mchezo wa kundi J wa kusaka tiketi ya fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022, uliopigwa na kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jana Jumanne (Septemba 07).

Mabao ya Stars katika mchezo huo yalifungwa na Erasto Nyoni, Feisal Salum na Novatus Dismas.

Kocha Poulsen amesema kuwa ni mafanikio makubwa kwa nchi kuongoza kundi baada ya mechi mbili kwakuwa ni jambo ambalo alijawahi kutokea nchini.

“Sote tumeshuhudia goli la mapema sana dhidi ya Madagascar lakini baada ya kupata bao la pili tumeona wachezaji wangu wakipoteza umakini kitu ambacho kiliwafanya wachezaji wa timu pinzani kurudi mchezoni na kufanikiwa kushinda magoli mawili mpaka muda wa mapumziko.”

”Tukiwa kwenye vyumba vya kubadilisha nguo sikua na budi na kuwambia wachezaji wangu kuwa waache kufanya makosa kwasababu tutaadhibiwa iwapo tutaendelea kupoteza mipira hasa katika eneo letu la hatari, nafurahia kuwa waliitikia wito wangu na baadaye kipindi cha pili tukapata bao la kuongoza na kutengeneza nafasi nyingi zaidi.”

”Natamani huu uwanja wa Benjamin Mkapa, uwe uwanja ambao tutashinda mechi zetu zote za nyumbani nikituamia kuwa ni kitu ambacho tutaendelea kukipambania.”

Ushindi wa mabao 3-2 unaiwezesha Taifa Stars kuongoza msimamo wa kundi J, lenye timu za Benin, DR Congo na Madagascar.

Taifa Stars imefikisha alama 4 sawa na Benin baada ya kucheza michezo miwili dhidi ya DR Congo uliomalizika kwa sare ya 1-1 na Madagascar uliomalizika kwa ushindi wa mabao 3-2.

Jamii yahitajika kuwatambua mahabusu,wafungwa kama sehemu ya jamii
RC Makalla: Wanaopangisha Magomeni Kota ni matapeli