Kocha wa Taifa Stars’ Kim Poulsen amesema kikosi chake kimejizatiti kukabiliana na Benin katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Kundi J wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Stars itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wake wa pili mfululizo kucheza Uwanjani hapo, baada ya kuibanjua Madagascar mabao 3-2.

Kocha Poulsen amesema wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo huo, baada ya kufanya mazoezi tangu Jumatatu (Oktoba 04).

Amesema wanaiheshimu sana Benin na atahakikisha kikosi chake kinacheza kwa nidhamu kubwa kesho Alkhamis (Oktoba 07), ili kutimiza lengo la kukusanya alama tatu muhimu.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunajiamini na tumejizatiti kukabiliana nao, na tunataka tudhihirishe ubora wetu tunapokuwa kwa Mkapa kabla hatujaenda kurudiana nao kwao baadae wiki hili.” amesema Kim Poulsen

Wakayi huo huo Mshambuliaji wa Taifa Stars John Bocco amezungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, ambapo amesema wapo vizuri na amewaomba watanzania kujitokeza uwanjani kwenda kuwaunga mkono.

Tayari Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethibitisha taarifa za kuruhusiwa kwa mashabiki 10,000 kuingia Uwanja wa Mkapa Kesho Alkhamis (Oktiba 07).

Kennedy Juma asivyokauka midomoni mwa wadau
Twiga Stars kuikabili Zambia