Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia Wananchi Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara waliokumbwa na janga la mafuriko, kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu na idara na taasisi zote kama walivyoagizwa chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu.
Kinana ameyasema hayo hii leo Desemba 4, 2023 wakati alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.
Aidha, Kinana pia amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu zao na waliojeruhiwa na kulazwa hopitalini kutokana na janga hilo ambapo amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema “mpaka sasa tumewapoteza ndugu zetu 57 katika maafa ya mafuriko eneo la Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara. Ndugu zetu wengine 85 waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Hospitali ya Wilaya ya Hanang na Kituo cha Afya Gendabi.”