Waziri mkuu aliyeondolewa madarakani nchini Sudan, bwana Abdalla Hamdok amesema serikali iliyoondolewa inaweza kufungua njia kwa taifa hilo kupata suluhu baada ya mapinduzi.

Wizara ya habari imesema waziri mkuu huyo alizungumza wakati wa mkutano na mabalozi akiwa nyumbani kwake.

Kumekuwa na maandamano dhidi ya mapinduzi katika mji mkuu na miji mingine kupinga mapinduzi hayo na Bwana Hamdok bado yuko kwenye kifungo cha nyumbani.

Baraza la mawaziri lilivunjwa baada ya mapinduzi Oktoba 25 na Jumuiya ya kimataifa imetoa wito kwa jeshi kuachia madaraka.

Video: Dakika 3 za Rais Samia COP 26
Rais Samia kuhutubia Mkutano wa COP 26