Rais Samia Suluhu Hassan leo Novemba 2, 2021 amehutubia katika mkutano wa 26 wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa unaojadili athari za mabadiliko ya Tabianchi.

Katika hotuba yake rais Samia ameeleza mikakati ya Tanzania ya kuhakikisha Nchi yake inakabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi ikiwa mojawapo ni kupanda miti kila sehemu ambayo imeathirika na mabadiliko hayo.

“Tumeweka mikakati mizuri ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, lakini hatuwezi kufanikiwa bila kupata uungwaji mkono madhubuti na kujengewa uwezo wa kitaalam,” ameongeza.

Pia Rais Samia amesema Tanzania ina mkakati maalumu wa kukabiliana na athari hizo ikiwa pamoja na kuomba nchi zote wanachama wa Umoja wa mataifa kuungana pamoja katika kukabiliana na athari hizi.

“Mabadiliko ya tabianchi ni suala la ulimwengu mzima, suluhisho lake linapaswa kuwa la ulimwengu mzima pia. Tunawaomba nchi zilizoendelea kutoa suluhisho na fedha za kutosha kutuwezesha sisi nchi zenye kipato cha chini kufanikisha malengo kwa namna endelevu,” amesema Rais Samia

Rais Samia ametoa Wito kwa Nchi zinazoendelea kuchua hatua za haraka kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kuhusika zaidi katika mikakati yote na kuongeza kuwa athari za mabadiliko ya Tabi ya nchi haya chagui nchi masikini wala nchi Tajiri.

Azam FC: Lwandamiza hajafukuzwa, hafukuzwi
Kiongozi alieondolewa madarakani Sudan anena