Aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ wakati wa Utawala wa Rais Jamal Emil Malinzi, (Eliud Mvela) ameingilia kati sakata la usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Tuisila Kisinda aliyesajiliwa Young Africans akitokea RS Berkane.

Ulingo wa Soka la Bongo umegubikwa na sakata la kiungo huyo baada ya TFF kuzuia usajili wake, kwa madai upo kinyume na utaratibu wa kikanuni, kufuatia Young Africans kutimiza idadi ya wachezaji 12 kwa msimu huu 2022/23.

Mvela amesema TFF inapaswa kuangalia kwa umakini suala la usajili wa Kisinda na kujiridhisha kama kuna ulazima wa kumzuia asiitumikie Young Africans.

Amesema kuna baadhi ya taratibu wa usajili kwa mchezaji huyo zilifuatwa huku akitolewa mfano wa kibali cha uhamisho wa kimataifa ‘ITC’ ambacho huagizwa na Shirikisho la Soka la nchi anayokwenda kucheza mchezaji.

“Iwapo Tuisila Kisinda alipata ITC, maana yake mfumo ulikubali na mchezaji hana tatizo hivyo ananafasi ya kupata leseni, Ila kwa kuwa Yanga wana Wachezaji (13) wa kimataifa, ni wajibu wa ‘TFF’ kuwaambia Yanga wapunguze mchezaji mmoja kisha taarifa iende ‘CAF’ kupitia TFF”

“Inawezekana hata Rais Wallace Karia anaumizwa na kuchukizwa na taarifa za Young Africans kuonewa lakini usikute tatizo ni kamati ambazo ni huru ambazo zinafanya maamuzi ya ajabu ajabu, Mfano ; Kufungia watu hovyo au waamuzi wanaochezesha hovyo huwezi kumlaumu Karia yeye hapulizi filimbi” amesema Eliud Mvela

Kenya: Kenyatta ajipanga kumkabidhi Ruto 'mikoba'
Kenya: Wafuasi wasema watamuapisha Odinga